Shirika la Msalaba Mwekundu na DCI kuimarisha ushirikiano

Tom Mathinji
1 Min Read
Shirika la Msalaba Mwekundu na DCI zaimarisha ushirikiano kuhusu haki na maswala ya kibinadamu.

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), imeelezea kujitole kwake kuimarisha ushirikiano na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC).

Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mohamed Amin, alisema ushirikiano huo utajumuisha ulinzi wa kijamii, upatikanaji wa haki na kutambua fursa mpya za ushirikiano.

Amin aliyasema hayo alipokuwa mwenyeji wa kiongozi wa ujumbe wa ICRC kanda ya Nairobi Marie Dubeau.

Kwenye mkutano huo, wawili hao walielezea kushirikiana katika mipango ya siku za usoni ambayo inapigia debe maadili ya kibinadamu na ushirikiano katika operesheni.

Kupitia ukurasa wa X, Amin alidokeza kwenye mkutano huo, taasisi hizo mbili zimejitolea kufanikisha utoaji wa huduma, kulinda heshima ya ubinadamu, majadiliano kwa manufaa ya raia wa Kenya.

Share This Article