Mwanamume mwenye umri wa miaka 55, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumdhulumu kimapenzi mwanawe wa kike.
Huku akikiri kosa hilo, mshtakiwa huyo alimwarifu Hakimu Mkuu Mkaazi E. Karani kwamba amemdhulumu mwanawe mara kadhaa na hata kumpachika mimba kati ya mwaka 2020 na 2024.
Mwanamume huyo ambaye alikuwa mbioni, alikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo alikubali mashtaka dhidi yake baada ya kusomewa mashtaka hayo.
Hata hivyo, alipopewa muda wa kujitetea, aliiomba mahakama hiyo kuzingatia kwamba hakupoteza muda wa mahakama.
Mahakama iliagiza kuwa mshukiwa huyo afanyiwe uchunguzi wa akili, ikizingatiwa kuwa anatuhumiwa kwa mauaji. Baadaye ilibainika kuwa anaweza kujibu mashtaka.