Ujenzi wa barabara ya safu mbili ya Rironi-Mau Summit kuanza mwezi Novemba

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto (Kulia) na rais wa kampuni ya ujenzi na mawasiliano ya China Zhang Bingman.

Ujenzi wa barabara ya safu mbili ya kilomita 170 ya Rironi-Naivasha-Mau Summit, utaanza Novemba 28, 2025.

Rais William Ruto, amesema ujenzi huo ni hatua kubwa katika kuimarisha uchukuzi wa abiria na mizogo kati ya Nairobi na Magharibi mwa nchi.

“Ujenzi huo utakomesha misongamano, ucheleweshwaji na ajali amabazo zimekuwa zikishuhudiwa,” alisema Rais Ruto.

Kiongozi wa taifa aliongeza kuwa siku hiyo hiyo, serikali itazindua ujenzi wa barabara ya safu mbili ya kilomita 58 ya Rironi-Maai Mahiu-Naivasha.

Rais aliyasema hayo leo Jumatatu aliposhiriki mazungumzo na rais wa kampuni ya ujenzi na mawasiliano ya China Zhang Bingman, katika Ikulu ya Nairobi. Kampuni hiyo imejukumiwa kujenga barabara hiyo.

“Maendeleo miundombinu yamesababisha taifa hili kupiga hatua, kutokana na ushirikiano thabiti kati ya Kenya, China na kampuni za Uchina,” aliongeza Rais Ruto.

Share This Article