Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliwalemea Nigeria mabao 4-3, kupitia penati na kufuzu kwa mchujo wa mwisho baina ya mabara kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao.
DRC maarufu kama the Leopards, walitoka nyuma na kulazimisha sare ya bao moja katika dakika 90, na baadaye ikabidi matuta yapigwe baada ya timu zote kutoshana nguvu.
Frank Onyeka aliwaweka Super Eagles uongozini kunako dakika ya tatu katika fainali hiyo iliyopigwa mjini Rabat,kabla ya Congo kusawazisha Meschack Elia dakika ya 32.
DRC watasubiri droo itakayobaini wapinzani wao katika mchujo wa mwezi Machi mwaka ujao huku wakipania kufuzu kwa mara ya kwanza kwa kombe la Dunia tangu wabadilishe jina kutoka Zaire.
Mataifa mengine yaliyofuzu kwa mchujo huo kutoka mabara mengine ni Jamaica, Honduras, Panama, Haiti, Costa Rica, Curacao, Suriname, Bolivia na New Caledonia.