Bingwa mara mbili wa Dunia na Olimpiki katika mbio za mita 5,000 na 10,000 Beatrice Chebet, siku ya Ijumaa alipokea Shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Kabianga kwa heshima na mchango wake katika Jamii.
Chebet alishinda dhahabu katika mbio za mita 5,000 na 10,000 katika mashindano ya Dunia yaliyoandaliwa mjini Tokyo,Japan mwezi Septemba mwaka huu.
Aidha, Chebet alishinda dhahabu mbili katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2024 jijini Paris Ufaransa.