Timu ya taifa ya Kenya kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 imeendeleza mazoezi yake mjini Adis Ababa, Ethiopia, kujiandaa kwa michuano ya CECAFA, kufuzu kwa fainali za kombe la AFCON.
Kenya chini ya ukufunzi wa kocha William Muluya, itafungua mechi hizo Novemba 18 dhidi ya Somalia, kabla ya kukabiliana na Rwanda tarehe 21 na Sudan Kusini siku tatu baadaye na hatimaye dhidi ya wenyeji Ethiopia Novemba 27.
Timu tatu bora kwenye mashindano hayo zitafuzu kwa kipute cha AFCON mwaka ujao.