Tuko tayari kwa chaguzi ndogo Novemba 27, wasema Polisi

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa Polisi wametangaza kuwa wako tayari kwa chaguzi ndogo za Jumatatu ijayo, Novemba 27, katika maeneo mbalimbali nchini.

Taarifa kutoka kwa huduma ya kitaifa ya Polisi NPS imesema kamwe haitakubali utovu wowote wa kiusalama na kuwataka wanasiasa kuzingatia sheria zilizowekwa.

Aidha, NPS imeapa kuwa haitapendelea mwanasiasa wala upande wowote wakati wa zoezi hilo na kuwataka wanasiasa hao, wafuasi wao na makundi yote kudumisha amani na kuendesha kampeni kwa ustaarabu.

IEBC imeratibu chaguzi hizo ndogo zikiwa za Useneta wa Baringo na maeneo bunge sita ya Banissa, Kasipul, Magarini, Malava, Mbeere North na Ugunja.

Pia, chaguzi hizo ndogo zitaandaliwa katika wadi 17 tofauti.

Share This Article