Rais Ruto akagua miradi ya maendeleo Kitui

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Alhamisi ameanza ziara ya kuzindua na kukagua miradi ya maendeleo katika kaunti ya Kitui.

Rais akiandamana na viongozi wa eneo la Ukambani amefungua soko la matunda na mboga la

Kamuwongo  lilojengwa na serikali ya kaunti ya Kitui,eneo la Mwingi .

Soko hilo litatumiwa na zaidi ya wafanyabiashara 200 na kutoa ajira kwa vijana na kuinua hali ya kichumi ya eneo.

Ruto aliandamana na Naibu wake Kithure Kindiki, Gavana wa kaunti hiyo Julius Malombe, Waziri wa Ardhi Alice Wahome, Waziri wa Leba Alfred Mutua na viongozi wengine wakiwemo Wabunge.

Awali Rais alitoa hatimiki 1,500 za vipande vya ardhi kwa wakazi wa maeneo ya Kamuwongo, Mwingi Kaskazini, kaunti ya Kitui.

Aidha, Ruto alizindua ujenzi wa barabara ya kilomita 13 ya Kamuwongo-Kandwia, itakayounganisha barabara ya Thika-Garissa kutoka mjini Mwingi .

Share This Article