Mbunge wa eneo bunge la Isiolo Kusini Tubi Bidu, ameaga dunia Jumatano jioni katika hospitali ya Nairobi alipokuwa akipokea matibabu.
Tubi alikuwa akihudumu kwa muhula wa kwanza bungeni baada ya kuchaguliwa, na awali alikuwa Spika wa kwanza wa bunge la kaunti ya Isiolo hadi mwaka 2017.
Akiwa bungeni mwenda zake alihudumu katika kamati za mazingira, misitu na uchimbaji madini na pia kamati ya kusikiza malalamishi ya umma.
Kifo cha Bidu kimetangazwa Jumatano jioni na Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula.