JD Vance aliahirisha ziara yake Kenya baada ya Marekani kujiondoa kwa kongamano la G20

Dismas Otuke
0 Min Read

Ziara iliyotarajiwa humu nchini ya Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance imeahirishwa kufuatia hatua ya Marekani kujiondoa kwa kongamano la G20 linalotarajiwa kuandaliwa nchini Afrika Kusini.

Kongamano la G20 limeratibiwa kufanyika mjini Johanesburg kati ya Novemba 22 na 23 mwaka huu.

Rais wa Donald Trump ametangaza bayana kuwa Marekani haitahudhuria kongamano hilo kutokana na hatua ya Afrika Kusini kuwabagua kirangi na kuwanyanyasa raia wa kigeni.

Share This Article