Rais Ruto: Tutaendelea kuunga mkono jamii ya Maa

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto akihutubu katika makala ya tatu ya sherehe za Maa kaunti ya Kajiado.

Rais William Ruto amesema serikali itaendelea kuunga mkono na kufanya kazi kwa karibu na jamii ya Maa, pamoja na kushirikiana na serikali za kaunti za Maa kuimarisha uhifadhi wa mazingira.

Akizungumza Jumamosi wakati wa makala ya tatu ya sherehe za Utalii na Utamaduni wa jamii ya Maa katika mbuga ya Amboseli kaunti ya Kajiado, kiongozi wa taifa alisema jamii ya Maa inasalia kuwa ishara ya utalii na ukumbusho wa amani kati ya binadamu na mali asili.

“Tunasherehekea jamii ya Maa, turathi iliyolindwa ambayo huenezwa kutoka kwa kizazi hadi kingine,” alisema Rais Ruto.

Rais aliongeza kuwa, kwa pamoja taifa hili linaweza kulinda mali asili na kuhakikisha kila mkenya ananufaika na utajiri unaotokana na shughuli za utalii.

Rais Ruto aliipongeza jamii ya Wamaasai kwa kuwa watunzaji wema wa ardhi, wanyamapori na utamaduni wao, akisema kuwa maeneo ambapo Wamaasai wanaishi ni bora akisema kuwa wamekuwa watunzaji wa mazingira ambayo bado yanavutia.

Share This Article