Rais William Ruto siku ya Jumamosi amekabidhi hifadhi ya kitaifa ya Wanyama ya Amboseli kwa kaunti ya Kajiado kutoka serikali ya kitaifa.
Haya yamejiri wakati Rais alipohudhuria sherehe za Jamii ya Maa katika mbuga ya wanyampori ya Amboseli.
Rais ametaja kuwa hatua hiyo itamaliza utata wa muda mrefu ambao umekuwepo kuhusu usimamizi wa hifadhi na kutambua uwezo na kujudi za jamii ya kaunti ya Kajiado kusimamia mbuga hiyo.

Hafla hiyo imeudhuriwa na uongozi wa kaunti ya Kajiado.