Harambee Stars imeratibiwa kucheza na Equatorial Guinea na Senegal katika mechi mbili za kujipima nguvu kuanzia Ijumaa ijayo Novemba 14.
Kenya itamenyana na Equatorial Guinea Novemba 14 uwanjani Emir mjini Antalya, Uturuki, kabla ya kukabiliana na Simba wa Teranga Senegal siku nne baadaye katika uga wa Mardan nchini Uturuki.
Mechi hizo za kirafiki kwa Kenya zimeratibiwa upya baada ya zile za awali dhidi ya Madagascar na Comoros kufutiliwa mbali.
Kocha wa Harambee Stars Benni McCarthy amefanyia mabadiliko kikosi chake akiwajumuisha kwa mara ya kwanza Kevin Otiende wa Nairobi United, Bryton Onyona wa Gor Mahia na Shariff Musa pia kutoka Gor Mahia kutwaa nafasi za Manzur Ali, Adam Wilson na Vincent Harper.
Harambee Stars inatarajiwa kuripoti kambini Jumapili Novemba 9 kujiandaa kabla ya kusafiri tarehe 12 mwezi huu.
Kikosi
Makipa
Byrne Omondi (Gor Mahia), Brian Bwire (Polokwane City), Brian Opondo (Tusker FC)
Mabeki
Sylvester Owino (Gor Mahia), Alphonce Omija (Etoile Du Sahel), Michael Kibwage (Gor Mahia), Ronney Onyango (Sogndal), Kevin Otiende (Nairobi United), Baron Ochieng (Zamalek), Bryton Onyona (Gor Mahia)
Viungo
Alpha Onyango (Gor Mahia), Duke Abuya (Yanga), Timothy Ouma (Lech Poznan), Marvin Nabwire (Kenya Police FC)
Washambulizi
Austine Odhiambo (Gor Mahia), William Lenkupae (VPS), Job Ochieng (Real Sociedad), Boniface Muchiri (Ulinzi Stars), Aldrine Kibet (Celta Vigo), Ovellah Ochieng (Nairobi United), Jonah Ayunga (ST Mirren), Ryan Ogam (Wolfsberger), Lawrence Okoth (SJK Seinajoki), Sharif Musa (Gor Mahia).