Kipchoge akutana na Rais Mstaafu Obama mjini New York

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara mbili wa Olimpiki katika mbio za marathoni Eliud Kipchoge siku ya Ijumaa amekutana na Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama mjini Washington, Marekani.

Obama na Kipchoge walijadiliana kuhusu njia za ushirikiano hususan katika michezo na ukuzaji talanta.

Kipchoge alimaliza wa 17 katika mbio zake za mwisho za marathoni katika mashindano ya New York Jumapili iliyopita.

Mwanariadha huyo anayejivunia muda wa pili kasi katika mbio za kilomita 42 ameshiriki marathoni kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Share This Article