Odemba atawazwa kocha bora Septemba katika tuzo za Betika/SJAK

Dismas Otuke
1 Min Read

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake ya soka Harambee Starlets , Beldine Odemba ametawazwa kocha bora wa chama cha Wanahabari wa michezo nchini SJAK kwa ushirikiano na kampuni ya kamari ya Betika katika mwezi wa Septemba.

Odemba ametawazwa Alhamisi katika uwanja wa kitaifa wa nyayo baada ya kuiongoza Starlets kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya pili miaka miwili tangu ateuliwe.

Kenya ilizishinda Tunisia na Gambia kabla ya kufuzu kwa kipute hicho kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2016.

Harambee Starlets itashiriki fainali za WAFCON nchini Morocco kati ya Machi 17 na Aprili 3 mwaka ujao.

Ili kutawazwa mshindi Odemnba amewashinda Kevin “Bling” Wambua wa Shujaa Coach, Musa Benjamin wa masumbwi, Nicholas Muyoti wa Nairobi United FC, Meshack Senge wa timu ya magongo, Simon Odongo wa Kenya Lionesses na Camilla Lydya wa triathlon

Fainali za WAFCON mwaka ujao kwa mara ya kwanza zitashirikisha mataifa 16 baada ya kuongezwa kutoka 12 na zitatumika kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2027.

Share This Article