Kalonzo awasili Opoda Farm na ng’ombe 100 kumwomboleza Raila

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amewasili katika shamba la Opoda mjini Bondo, kaunti ya Siaya na fahali  100 siku ya Alhamisi kumwomboleza mwandani wake wa kisiasa hayati Raila Odinga.

Kalonzo akiandamana na Magavana wa kaunti za Ukambani, wakiwemo  Wavinya Ndeti wa Machakos na Mutula Kilonzo Junior wa Makueni na viongozi wengine, wamepokelewa na Gavana wa Siaya James Orengo.

Wakiwa shambani kwa Raila Kang’o ka Jaramogi, viongozi hao wametoa heshima zao kwa kaburi la Raila baada ya kukaribishwa na Raila Junior pamoja na mjane, Mama Ida Odinga.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Kalonzo alitaja hatua za ukombozi za kushinikiza Kenya bora wakati alipofanya kazi kwa pamoja na Raila wakiwa upinzani.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Kalonzo kurejea nyumbani kwa Raila tangu mazishi ya Oktoba 19.

 

Share This Article