Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari ya kiusalama kwa raia wake walio nchini Tanzania kufuatia machafuko yaliyotokea maajuzi baada ya uchaguzi mkuu wa mwishoni mwa mwezi jana.
Licha ya hatia ya kutotoka nchi kuondolewa katika mji mkuu wa Dar es Salaam, miji mingine ingali na kafyu huku idadi kubwa ya maafisa wa polisi wakishika doria.
Ubalozi huo umeongeza kuwa usafiri ungali changamoto katika maeneo mengi huku maafisa wa usalama wakiwachunguza watu katika maeneo mengi na kukamatwa kwa muda kwa baadhi ya watu.
Marekani imewataka raia wake kujiepusha kushiriki maandamano, maeneo yaliyo na misongamano, na kufuatilia kwa karibu yanayojiri kupitia vyombo vya habari nchini Tanzania.
Arifa hiyo pia imekiri kuwepo kwa changamoto ya kufanya miamala kupitia mitandao huku huduma nyingi za internet zikiwa bado zimefungwa au kubanwa.
Imeripotiwa kuwa polisi wanafanya misako ya kutwaa vifaa meme vya raia kama njia ya kuzuia usambazaji wa video na picha zinazozua hofu kwa wananchi.