Rais William Ruto amekariri kujitolea kwake kwa serikali yake kuimarisha uzalishaji mifugo kupitia mfumo wa kiuchumi wa Bottom Up ili kuwanufaisha wakulima.
Rais amesema haya kwenye ziara yake nchini Qatar, alipozuru mojawapo wa miradi mikubwa zaidi ya ufugaji mifugo mjini Doha.
Ruto amesema serikali yake imeongeza uuzaji wa bidhaa za mifugo nje ha nchi kwa asilimia 45 katika muda wa miaka mitatu iliyopita.
Kenya pia ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazoongoza kwa maziwa , ikitoa lita bilioni 5.3 kwa mwaka.
Hata hivyo, Ruto alikiri kuwa kungali na changamoto ambapo kati ya maziwa yote yanayizalishwa humu nchini, ni asilimia 30 pekee yanayochakatwa kutokana na ukosefu wa miundombinu ya kutosha.
Katika ziara yake nchini Qatar, Rais alizuru kiwanda kikubwa zaidi cha uzalishaji mifugo cha Baladna Food Industries, mjini Al Khor, ambacho kina kuku na ng’ombe 24,000 wanaotoa maziwa lita laki nne kwa siku.