Cameroon,Mali,Misri na Ivory Coast zimefuzu Kwa fainali za Kombe la Afrika Kwa wanawake (WAFCON) mwaka ujao nchini Morocco.
Hii ni kufuatia hatua ya shirikisho la soka Afrika CAF kuongeza idadi ya timu zinazoshiriki kipute hicho kutoka 12 hadi 16 kuanzia mwaka ujao.
Aidha, CAF ilichagua timu hizi nne zilizoshindwa katika hatua ya mwisho ya kufuzu kwa kuzingatia msimamo wao wa FIFA.
Makala ya mwaka ujao ya WAFCON yataandaliwa nchini Morocco kati ya Machi 17 na Aprili 3 na yatatumika kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2027.