Wakenya 184 kutoka sekta mbalimbali wametuzwa katika halfa za mwaka huu za kusherehekea siku kuu ya Mashujaa, zilizoandaliwa katika uwanja wa Ithookwe kaunti ya Kitui.
Waliotuzwa ni pamoja na wanamichezo, wanahabari, wanasayansi, watafiti, wanamazingira na wapiganiaji haki za kibinadamu miongoni mwa wengine.
Wanamichezo waliotambuliwa ni pamoja na wachezaji soka wa Harambee Stars Ryan Ogam, Aboud Omar, Byrne Omondi na Alpha Onyango, na Milred Cheche.
Wanariadha waliowawa ni aliyekuwa kocha wa mwanariadha marehemu Kelvin Kiptum, marehemu Gervais Hakizimana, Clinton Aluvi na Cynthia Chepkurui.