Chama tawala nchini Zimbabwe ZANU-PF kimetangaza kuanzisha mikakati ya kuongeza utawala wa Rais Emerson Mnangagwa kwa mihula miwili zaidi.
Hii ina maana kuwa Rais huyo aliye na umri wa miaka 83 atasalia uongozini hadi mwaka 2030.
Chama tawala cha ZANU–PF kimekuwa madarakani tangu mwaka 1980.
Kulingana na katiba ya sasa, Mnangagwa alipaswa kuondoka afisini mwaka 2028 baada ya kuhitimisha mihula ya miaka mitano kila mmoja, ilivyo kwa katiba ya sasa.