Sherehe za siku kuu ya Mashujaa kuandaliwa leo kaunti ya Kitui

Marion Bosire
1 Min Read

Sherehe za siku kuu ya Mashujaa zitaandaliwa leo katika uwanja wa michezo wa Ithookwe katika kaunti ya Kitui, chini ya uongozi wa Rais william Ruto.

Awali kulikuwa na wasiwasi kati ya wananchi kuhusu iwapo sherehe hizo zitaandaliwa kufuatia tangazo la Rais William Ruto la siku saba za maombolezi ya kitaifa kufuatia kifo cha waziri mkuu wa zamani Raila Amolo Odinga.

Msemaji wa serikali Isaac Mwaura alithibitisha maandalizi ya sherehe hizo kupitia taarifa ambapo alimtaja Raila Odinga kuwa shujaa na kiongozi ambaye alikuwa sehemu kubwa ya safari ya taifa la Kenya.

Mwaura alielezea kwamba siku kuu ya mashujaa ni muhimu sana kulingana na sheria ya siku kuu za kitaifa katika katiba ya mwaka 2010 na ni lazima wananchi watambue mashujaa wao.

Hata hivyo kuna shughuli kadhaa zinazoambatana na sherehe hizo ambazo zimeahirishwa kama vile wiki ya kawi na kikao cha kiamasha kinywa na wanahabari.

Marehemu Raila Odinga anatarajiwa kuwa mmoja wa mashujaa ambao wataenziwa hii leo kwenye uwanja huo wa Ithookwe katika kaunti ya Kitui.

Tayari mgeni mashuhuri wa sherehe hizo ambaye ni Rais wa Senegal Bassirou Faye amewasili nchini kwa ajili ya maadhimisho ya leo ya siku kuu ya Mashujaa.

Share This Article