Mwili wa Raila wazikwa Bondo kaunti ya Siaya

Tom Mathinji
1 Min Read

Vikosi vya Ulinzi Nchini KDF, vilifyetua risasi 17 kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, aliyezikwa Jumapili Bondo, Kaunti ya Siaya.

Mwili wa Raila uliteremshwa kaburini muda mfupi baada ya saa kuni na moja jioni katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa wakuu serikalini, familia na wageni wachache walioalikwa.

Raila Odinga alizikwa kuambatana na taratibu za kijeshi, baada ya Rais William Ruto kutangaza kuwa mazishi ya kiongozi huyo wa chama chama cha ODM yatakuwa ya kitaifa.

Jeneza lililokuwa na mwili wa Raila na ambalo lilifunikwa kwa bendera ya Kenya, liliteremshwa katika  makaburi ya Kang’o ka Jaramogi, alikozikwa babake Jaramogi Oginga Odinga na mamake Mary Odinga.

Raila alifariki Jumatano Oktoba 15,2025 akipokea matibabu nchini India.

Share This Article