ODM itakuwa ndani ya serikali ijayo, asema Ruto

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amesema chama cha ODM kilichoongozwa na marehemu Raila Odinga kitakuwa ndani  ya serikali ijayo mwaka 2027.

Akihutubu katika mazishi ya marehemu Raila, Ruto amesema kamwe hatakubali watu wabinafsi kukitumia chama hicho kwa maslahi yao.

Ruto amefichua ili kaufikia azma ya marehemu Raila atahakikisha kuwa chama cha ODM aidhja kitabuni serikali ijayo ama kitakuwa ndani ya serikali.

Aidha Ruto  kwa mara ya kwanza amemtaja Raila kuwa Rais wa wananchi.

Share This Article