Misa ya marehemu Raila Odinga itafanyika katika chuo kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga mapema Jumapili kabla ya mazishi.
Baada ya ibada hiyo, mwili wa Hayati Raila utazikwa katika kaburi la familia maarufu kama Kang’o Ka Jaramogi.
Mwili wa marehemu Raila utazikwa kando na kaburi la marehemu babake Jaramogi Oginga Odinga.