Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga umewasilishwa nyumbani kwake Bondo.
Ndege ya jeshi iliyoubeba mwili wa Raila ilitua nyumbani kwa Raila Bondo kaunti ya Siaya mida ya saa kumi na dakika 16 alasiri.
Waombolezaji waliojawa na simanzi waliupokea mwili wa hayati Raila huku wengine wakishindwa kujistahimili.
Mwili huo utalazwa nyumbani kwake katika shamba la Opoda kabla ya mazishi ya Jumapili.