Lupita Nyong’o amuomboleza Raila Odinga

Tom Mathinji
1 Min Read

Mshindi wa tuzo katika sanaa ya uigizaji Lupita Nyon’go, amejiunga na wakenya na ulimwengu kwa jumla kumuomboleza aliyekuwa Waziri Mkuu hayati Raila Odinga.

Kwenye taarifa yake, muigizaji huyo alimkumbuka Raila kama shujaa wa kupigiwa mfano.

“Najiunga na Wakenya kumuomboleza hayati Raila Odinga. Nilimjua kwa kuwa alikuwa rafiki wa karibu sana wa babangu mzazi, na pia kama shujaa wa taifa hili,” alisema Nyong’o.

Lupita alisema Raila alimsaidia sana babake na familia yao kwa jumla, akichangia katika ufanisi wa familia hiyo.

“Alimshikilia babangu na kushikilia familia yetu nyakati za furaha na pia nyakati za changamoto, nasi pia tukampa mkono huo huo,” aliongeza mwigizaji huyo.

Lupita aliifariji familia mzima ya Odinga, akiiombea utulivu na faraja wakati huu mgumu wa majonzi.

“Pumzika vyema mjomba Raila. Natuma faraja zangu Kwa familia nzima ya Odinga, wakati huu mgumu wa majonzi,” alisema Lupita.

Share This Article