Kalonzo azuru Karen kuomboleza na familia ya Raila

Tom Mathinji
1 Min Read
Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka azuru Karen kuomboleza na familia ya Raila Odinga.

Kiongozi wa chama cha Wiper Stephen Kalozo Musyoka, Ijumaa alasiri alizuru nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, kuomboleza na Mama Ida na familia yake.

Kalonzo alimtaja Raila kuwa kiongozi mwenye ujasiri, huku akiishukuru familia ya Odinga kwa kumpa fursa Raila kulihudumia taifa hili.

“Familia ya Odinga iligawana nasi kiongozi huyo, kiasi kwamba Raila alikuwa nguzo kuu katika kizazi kilichozingatia haki na umoja wa Kenya,” alisema Kalonzo kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa X.

Makamu huyo wa zamani wa Rais, aliahidi usaidizi wake pamoja na maombi kwa familia ya Odinga, akiwahakikishia kuwa atawaunga mkono wakati huu mgumu wa majonzi.

“Familia ya Odinga kwa sasa inahitaji usaidizi wetu…. Mama Ida unapoomboleza, kuwa na amani ukifahamu kuwa maisha ya Baba yalikuwa ya kusudi na kujitoa mhanga,” aliongeza kiongozi huyo wa Wiper.

Kalonzo alitoa wito kwa Wakenya kuheshimu urithi ambao Raila alipigania.

Raila Odinga atazikwa nyumbani kwao Bondo, kaunti ya Siaya.

Share This Article