Polisi akamatwa baada ya mwanamke kupigwa risasi Homa Bay

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanamume awaua wanawe wawili kabla ya kujitoa uhai Mai Mahiu.

Afisa wa polisi anazuiliwa baada ya mwanamke kupigwa risasi nje ya kituo cha polisi cha Homa Bay Alhamisi usiku.

Kisa hicho kilitokea wakati umati ulikuwa umekusanyika kumuomboleza aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Homa Bay Jashon Odhiambo Pollo, alisema kisa hicho kilitokea wakati umati huo ulijaribu kuingia ndani ya kituo hicho cha polisi.

Kulingana na kamanda huyo, maafisa wa polisi waliokuwa zamuni, walijaribu kutuliza umati huo, huku wengine wakiwarushia mawe maafisa hao wa polisi.

Ni wakati wa purukushani hizo ambapo Yvonne Lucy alipigwa risasi akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake. Alipelekwa hospitalini lakini alifariki akiendelea kupokea matibabu.

“Afisa huyo wa polisi sasa anazuiliwa huku uchunguzi ukianzishwa na maafisa wa Halmashauri ya Kutathmini Utendakazi wa Polisi (IPOA), na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Tukio hilo lilijiri huku wakenya wakiendelea kumuomboleza aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, aliyefariki Jumatano asubuhi akipokea matibabu nchini India.

Raila atazikwa nyumbani kwao Bondo kaunti ya Siaya siku ya Jumapili.

Share This Article