Rais William Ruto amemtaja marehemu Raila Odinga kuwa kiongozi wa kuigwa na aliyejitolea kulihudumia taifa kwa moyo na ari yake yote.
Ruto amesema walishirikiana vyema na marehemu Baba na alisimama naye wakati mgumu ambapo taifa lilikaribia kuporomoka mwaka jana.
Kiongozi wa nchi amesema azma ya Raila ya kuwa na Kenya bora itasalia daima miongoni mwa Wakenya licha yake kufariki.
Aidha, Ruto amemtaja marehemu Raila kuwa kiongozi ambaye hatawahi kuwepo tena humu nchini katika karne zijazo.
Rais alikuwa akiwatubia waombolezaji katika ibada ya mazishi ya kitaifa ya Raila katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.