Kitinda mimba wa marehemu Raila Odinga, Winnie Odinga, amewafurahisha waombolezaji waliofika katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo, akimtaja babake kuwa alikuwa mwenye bashasha na busara tele.
Winnie ambaye ni Mbunge katika bunge la Afrika Mashariki (EALA) amesema vitendawili alivyokuwa akighani marehemu Raila katika mikutano ya kisiasa alikuwa akivifanyia majiribio akiwa nyumbani na wanawe.
Aidha amewapongeza Wakenya kwa kusimama na familia yao wakati huu mgumu wa kuomboleza kifo cha babake.