Raila alichukia ulafi,ufisadi na uongo, asema mama Ida

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Amolo Odinga alichukia ufisadi, ulafi na udanganyifu.

Akiwahutubia waombolezaji katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo katika ibada ya marehemu Raila, mkewe Ida Odinga amesema kuwa maono ya Raila yalikuwa kupigana dhidi ya maovu ya kijamii.

Ida amesema kifo chake Rail ni pigo kubwa sio tu kwa familia bali pia kwa taifa zima kutokana na idadi kubwa ya wafuasi.

Mama Ida amewaomba pia Wakenya kudumisha amani kama njia ya kumuenzi Raila.

Share This Article