Raia wa Kisumu kuutazama mwili wa Raila Jumamosi

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga aliyefariki wakati akipokea matibabu nchini India

Raia wa Kisumu watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga siku ya Jumamosi.

Mwili huo utawasilishwa katika uwanja wa ndege wa kaunti ya Kisumu mapema Jumamosi kabla ya kupelekwa katika uwanja wa  michezo wa Moi.

Wananchi watautazama mwili wa Raila kuanzia saa tatu na dakika 20 asubuhi hadi saa nane adhuhuri.

Baadaye mwili utapelekwa nyumbani kwa marehemu mjini Bondo kwa mkesha kabla ya mazishi ya Jumapili.

Share This Article