EPRA yadumisha bei za Mafuta

Tom Mathinji
1 Min Read
EPRA yadumisha bei za Mafuta.

Halmashauri ya kudhibiti Nishati na Mafuta nchini (EPRA), imedumisha bei ya mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta Taa, kwenye tathmini yake ya hivi punde.

Hatua hiyo inamaanisha kwamba lita moja ya mafuta ya Super itaendelea kuuzwa kwa shilingi 184.52, huku Dizeli ikiuzwa kwa shilingi 171.47 na mafuta taa kwa shilingi 154.78 Jijini Nairobi.

Jijini Mombasa, lita moja ya mafuta ya Super itauzwa shilingi 181.24, Dizeli ikuzwa shilingi 168.19 nayo Mafuta Taa ikiuzwa Shilingi 151.49.

Bei hizo zinajumuisha ushuru ziada wa thamani, (VAT) wa asilimia 16 kuambatana na kanuni za sheria ya fedha ya mwaka 2023, sheria ya marekebisho ya ushuru ya mwaka 2024 na viwango vipya vya ushuru wa forodhani uliobadilishwa kuambatana na mfumko wa bei.

EPRA ilisema kuwa bei za rejareja za bidhaa za mafuta ambazo tayari ziko humu nchini hudhibitiwa ili kuhakikisha wateja wanazinunua kwa bei nafuu.

TAGGED:
Share This Article