Morocco ilishinda itachuana na Marekani katika robo fainali kali ya kuwania Kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 inayoendelea nchini Chile.
Morocco ndiyo timu pekee ya Afrika kufuzu kwa hatua ya nane bora baada ya kuwazidia maarifa Korea Kusini kwa mabao 2-1 mapema Ijumaa.
Awalia Marekani ilifuzu pia baada ya kucharaza Italia magoli 3-0.
Robo fainali ya kwanza itasakatwa Jumamosi Uhispania wakikabiliana na Colombia, kabla ya Argentina kumenyana na Mexico mapema Jumapili.
Morocco watakabana koo na Marekani Jumapili usiku kisha Norway wakamilishe ratiba dhidi ya Ufaransa.