Rais William Ruto leo anatarajiwa kufunga rasmi kongamano la 24 la soko la pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) kwa kikao cha viongozi wa mataifa wanachama.
Ruto anatarajiwa kukabidhiwa rasmi uenyekiti wa COMESA kutoka kwa Rais wa Burundi Everest Ndayishimiye.
Kongamano hilo ambalo limekuwa likiendelea tangu Jumatatu wiki hii limewaleta pamoja wajasiriamali, wadau mbalimbali wa kibiashara na viongozi wa serikali za mataifa wanachama.