Ni vita vya panzi Kenya ikichuana na Burundi leo kufuzu Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Harambee Stars itachuana wenyeji Burundi leo saa kumi Alasiri katika uwanja wa Intwanari katika mchuano wa mzunguko wa tisa kundini F, kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao.

Timu zote zitacheza mechi ya kuheshimu ratiba tu kwani hazina nafasi ya kufuzu, Burundi ikiwa na alama 10, moja zaidi ya Kenya.

Kenya na Burundi zilitoka sare katika mchuano wa mkumbo wa kwanza ulioandaliwa mwaka jana nchini Malawi.

Pambano hilo litarushwa mubasahara kupitia runinga ya taifa KBC Channal 1.

Share This Article