EACC yamkamata afisa wa NCWSC kwa kughushi cheti ya masomo

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa akamatwa kwa kughushi cheti cha masomo.

Tume ya Madili na vita dhidi ya Ufisadi EACC, imemkamata na kumfikisha mahakamani mfanyakazi mmoja wa kampuni ya Maji na Mabomba ya Majitaka ya Nairobi (NCWSC) kwa kugushi cheti cha mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE alichokitumia kupata ajira.

Michael Kilonzo Mauluko anadaiwa kuwasilisha cheti hicho gushi alichosema alipokea kutoka shule ya upili ya Bishop Ndingi.

Kukamatwa kwa Kilonzo kufuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na maafisa wa EACC baada ya kupokea habari kuhusu cheti hicho cha kutatanisha mwaka 2023.

Uchunguzi ulipokamilika, mshukiwa huyo alifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka kughushi, udanganyifu na kuwasilisha cheti bandia.

Hata hivyo, alikanusha mashtaka hayo na kuwachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu shilingi laki moja.

Kesi hiyo itatajwa Oktoba 22.

TAGGED:
Share This Article