Washukiwa saba washtakiwa kwa kuilaghai SHA shilingi milioni 7

Tom Mathinji
2 Min Read
Washukiwa saba washtakiwa kwa kuilaghai SHA shilingi milionin 7.

Washukiwa saba walifikishwa katika mahakama ya Milimani wakikabiliwa na mashtaka ya kuilaghai Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) shilingi milioni 7.

Mahakama iliwapata saba hao na makosa ya kupata fedha kwa njia ya uhalifu, udanganyifu,na uwasilishaji stakabadhi bandia.

Washukiwa hao ni pamoja na Markdhillion Mutsotso, ambaye ni mfanyakazi wa kituo cha afya cha St. Mark Orthodox, Patrick Kanya na Faith Chepkurui, wakurugenzi wa kituo cha afya cha, Jambo Jipya  Steven Okinyi na Justine Baraka, ambao ni maafisa wa kliniki, Pauline Wanjiru, ambaye ni muuguzi na Naida Mbeyu.

Kulingana na uchunguzi, Kanya, Chepkurui, Okinyi, Baraka, Wanjiru, na Mbeyu, wanadaiwa kuwasilisha stakabadhi bandia katika kituo cha afya cha Jambo Jipya katika kaunti ya Kilifi na kusababisha malipo haramu ya shilingi 2,032,680 kati ya mwezi November 2024 Juni 2025.

Mahakama iliwaachilia Kanya na Chepkurui dhamana ya shilingi 600,000, huku Okinyi, Baraka, Wanjiru, na Mbeyu wakiachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000.

Katika kesi sawa na hiyo, Mutsotso alishtakiwa kwa kuilaghai SHA shilingi 5,128,400 kupitia malipo ya uwongo yaliyotayarishiwa katika kituo cha afya cha St. Mark Orthodox kilicho Chavakali, kaunti ya Vihiga County, kati ya mwezi Oktoba 2024 na Juni 2025. Aidha aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000.

Mahakama hiyo ilitoa kibali cha kukamatwa kwa Fenley Ngairah, ambaye ni mkurugenzi wa St. Mark Orthodox Sammy Otieno.

Kesi hiyo itatajwa Oktoba 21, 2025.

TAGGED:
Share This Article