Zoezi la kitaifa la kuwasjili wapiga kura laingia siku ya pili

Martin Mwanje
1 Min Read
Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku akiwa na Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon wakati wa uzinduzi wa zoezi la usajili wa wapiga kura

Zoezi endelevu la kuwasjili wapiga kura limeingia siku ya pili leo Jumanne huku idadi ndogo ya Wakenya wakijitokeza kujiandikisha kama wapiga kura. 

Ni makumi ya watu tu waliojitokeza kujisajili kama wapiga kura wakati wa zoezi hilo la kitaifa lililozinduliwa hiyo jana katika kaunti ya Kajiado.

Ni hali ambayo imeifanya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini  (IEBC) kutoa wito kwa Wakenya kutumia fursa hii kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha kama wapiga kura.

IEBC inasema itaendesha zoezi hilo katika maeneo bunge yote 290 na vituo 57 vya Huduma Centre ili kuhakikisha watu wengi wanajisajili.

Hata hivyo, zoezi hilo kwa sasa halitaendeshwa katika maeneo 24 ambako chaguzi ndogo zitaandaliwa Novemba 27.

IEBC badala yake inasema zoezi la kuwasajili wapiga kura katika maeneo hayo litaandaliwa baada ya chaguzi hizo.

Tume hiyo inalenga kuwasajili hadi wapiga kura milioni 28.5 kufikia mwaka 2027 utakapoandaliwa uchaguzi mkuu nchini.

 

Share This Article