Rais Ruto: Kenya na Italia zimekuwa na uhusiano mwema wa kidiplomasia

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto na Balozi wa Italia anayeondoka hapa nchini Roberto Natali (Kulia).

Rais William Ruto amesema Kenya na Italia zimekuwa na uhusiano mwema wa kidiplomasia kwa muda wa miongo sita.

Kulingana na Rais Ruto, uhusiano huo ulijikita pakubwa katika biashara, uwekezaji, elimu, afya, kilimo, utamaduni na uhusiano baina ya raia wa nchi hizo mbili.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo Jumatatu, kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa X, alipomuaga balozi wa Italia Roberto Natali ambaye muda wake wa kuhudumu hapa nchini umekamilika.

Kwenye ujumbe huo, Rais alisema Kenya iko tayari kushirikiana na Italia kutekeleza mpango wa Mattei Barani Afrika, ambao unapiga jeki ushirikiano katika kawi, miundombinu na afya.

Aidha, Rais Ruto alimpongeza balozi huyo kwa kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili, huku akimtakia heri njema katika siku zake za usoni.

Share This Article