Kampeni zachacha Cameroon tayari kwa uchaguzi mkuu Oktoba 12

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampeni za kisiasa zimeingia siku ya tatu nchini Cameroon siku ya Jumatatu, huku uchaguzi mkuu ukiratibiwa kuandaliwa Oktoba 12 mwaka huu.

Rais Paul Biya, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 43, anawania muhula mwingine.

Hata hivyo Rais Biya anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa waaniaji kadhaa akiwemo mwandani wake wa zamani ambaye alikuwa Waziri wa Utalii Bello Bouba Maigari na Issa Tchiroma Bakary anayetarajiwa kuzindua kampeni yake wiki hii.

Waaniaji wa upinzani wanapiga njama ya kuungana na kumwasilisha mgombezi mmoja atakayekabiliana na Rais Biya.

Takriban wapiga kura milioni 8 wamejiandikisha kwa uchaguzi huo ambapo Biya, mwenye umri wa miaka 92 na rais mkongwe zaidi duniani, anawania muhula wa nane.

 

Share This Article