Tusker FC waleweshwa na Matarishi Posta

Dismas Otuke
1 Min Read

Masaibu ya mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Kenya, Tusker FC, yameendelea Jumamosi baada ya kupoteza mechi ya pili mtawalia waliponyukwa na Posta Rangers mabao 2-1, katika uwanja wa Dandora.

Lokuwam Eliud alipachika magoli yote kwa wenyeji Posta kunako dakika ya 3 na 25, kabla ya Erick Kapaito kukomboa moja dakika ya 35.

Ulikuwa ushinde wa pili kwa Tusker baada ya kuambulia kichapo cha 2-0 dhidi ya KCB katika mchuano wa ufunguzi wiki jana.

Kakamega Homoboyz walitoka sare tasa Mara Sugar katika mchuano mwingine wa raundi ya pili uliosakatwa Jumamosi.

Share This Article