Bingwa wa Olimpiki katika marathon Alphonce Felix Simbu amepandishwa cheo katika jeshi la Tanzania kufuatia matokeo bora katika mashindano ya Riadha Duniani mjini Tokyo, Japan.
Simbu amepandishwa cheo kutoka wadhfa wa Sergeant hadi Staff Sergeant baada ya kushinda dhahabu ya mbio za 42 katika mashindano ya Riadha Duniani.
Mkuu wa majeshi ya Tanzania John Mkundi alimpandisha Simbu cheo katika hafla iliyoandaliwa jijini Dar es Salaam.
Simbu ndiye Mtanzania wa kwanza kunyakua dhahabu ya mashindano ya Riadha Duniani.