Weasel Manizo na mkewe wapigana tena

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Uganda Douglas Mayanja maarufu kama Weasel Manizo na mke wake Sandra Teta, wanaripotiwa kupigana tena, yapata miezi miwili tu tangu ugomvi wao kuishia pabaya.

Video ilisambazwa mitandaoni jana inayomwonyesha Weasel akilia akiomba usaidizi huku watu wa familia yake wakimzuia Sandra aliyekuwa na hasira asimpige.

Katika video hiyo Weasel anasikika akisema, “Huyu ndiye mtu alinikanyaga kwa kutumia gari. Mnaona vile huwa ananichukulia?” huku Sandara akisikika akikana madai ya kumuumiza Weasel.

Msanii huyo anaendelea kulia kwenye hiyo video akimwita kakake mkubwa Chameleone, akimtaka amwondolee Sandara anayemtaja kuwa ‘Mrwanda’ kwani ana hofu kwamba atamuua.

Kaka huyo mdogo wa Chameleone anasikika pia akimtaka Sandra aondoke nyumbani kwao arejee kwenye nyumba yao.

Mwezi Julai, wawili hao waligonga vichwa vya habari nchini Uganda baada ya Sandra kudaiwa kumgonga Weasel kwa kutumia gari katika baa moja eneo la Munyonyo.

Weasel alipelekwa katika hospitali ya Nsambya akiwa amevunjika mguu na Sandra akakamatwa na maafisa wa polisi. Aliachiliwa muda mfupi baadaye kufuatia ombi la Weasel ambaye alisema hakuwa na nia ya kumshtaki.

Share This Article