Idara ya Polisi yawapokea mabingwa wa Dunia kutoka Tokyo

Kenya ilimaliza ya pili kwenye msimamo  wa dunia na ya kwanza barani Afrika kwa dhahabu 7, fedha 2 na shaba 2.

Dismas Otuke
1 Min Read
Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Eliud Lagat akiwa na mabingwa wa Dunia Faith Kipyegon na Beatrice Chebet

Idara ya Kitaifa ya Huduma za Polisi, NPS, iliwapokea Mabingwa wa Dunia na Wanariadha wa Polisi waliorejea nchini Jumanne, baada ya kushiriki mashindano ya Riadha Duniani jijini Tokyo, Japani.

Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Eliud Lagat aliwapokea mabingwa wa Dunia Faith Kipyegon na Koplo Beatrice Chebet katika makao ya polisi, jumba la Vigilance.

Chebet alinyakua dhahabu mbili za mita 5,000 na mita 10,000, huku Kipyegon akinyakua dhahabu ya mita 1,500 na nishani ya fedha ya mita 5,000.

Lagat alitangaza kuanzishwa kwa mchakato wa kupandishwa cheo kwa Chebet hadi kiwango cha Sajini, huku akiipongeza timu ya Kenya kwa kusajili matokeo bora jijini Tokyo.

Kenya ilimaliza ya pili kwenye msimamo  wa dunia na ya kwanza barani Afrika kwa dhahabu 7, fedha 2 na shaba 2.

Share This Article