Polisi kufanya usajili wa makurutu ngazi ya konstebo mwezi Oktoba

Dismas Otuke
1 Min Read

Idara ya Kitaifa ya Polisi itafanya zoezi la usajili wa makurutu wa ngazi ya konstebo katika vituo 416 kote nchini baina ya tarehe 3 na 9 mwezi ujao wa Oktoba.

Kulingana na tangazo hilo, usajili utaandaliwa katika kaunti zote 47 nchini, huku wanaopania kujiunga na idara hiyo wakihitajika kuwa kati ya umri wa miaka 18 na 28.

Aidha, ni sharti wawe na alama ya wastani ya D+ katika mtihani wa kidato cha nne, KCSE na pia alama sawa kwa lugha za Kiingereza na Kiswahili.

Wanaume pia wapaswa kuwa na kimo kisichopungua futi 5 na inchi 8 huku wanawake wakihitajika kuwa na kimo kisichopungua futi 5 na inchi 3.

Jumla ya vituo 416 katika kaunti zote 47 nchini vimetengewa zoezi hilo  la siku saba.

Share This Article