Kenya imekafiri kuendelea kushirikiana na Canada katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya nchi hizo mbili.
Rais William Ruto amesema haya siku ya Jumanne alipokutana na Waziri Mkuu wa Kanada Mark Carney mjini New York, Marekani, pembezoni mwa mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Ruto amesema wameafikiana kuimarisha ushirikiano katika mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha mazingira.