Davido ateuliwa mwanachama wa Grammy

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa mtindo wa Afrobeat kutoka Nigeria Davido ameteuliwa kuwa mwanachama wa akademia ya Grammy, na hivyo kumpa uwezo wa kushiriki shughuli ya kupiga kura katika tuzo za Grammy.

Hatua hii ni mafanikio makubwa kwa Davido na mtindo wa Afrobeats kwa jumla, kwani inazidi kuthibitisha mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa Afrika kimataifa.

Grammy Recording Academy hupokea wanachama Kutoka idara mbalimbali za tasnia ya muziki kama wasanii, watayarishaji muziki, waandishi wa nyimbo, mameneja wa muziki na wengine.

Ujumuishaji huo unalenga kuhakikisha kwamba shughuli ya kupiga kura inahusisha wataalamu wa tasnia ya muziki.

Wasanii watakaopitishwa kuwania tuzo zijazo za Grammy katika vitengo mbali mbali watatangazwa rasmi Ijumaa, Novemba 07, 2025, huku hafla ya kugawa tuzo zenyewe ikifanyika February 1, 2026 Katika Ukumbi Wa Crypto Jijini Los Angeles, Nchini Marekani.

Share This Article