Ufaransa yalitambua taifa la Palestina

Martin Mwanje
1 Min Read
Emmanuel Macron - Rais wa Ufaransa

Ufaransa imetangaza rasmi kulitambua taifa la Palestina. 

Tangazo hilo lilitolewa na Rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron kwenye hotuba yake katika Umoja wa Mataifa, UN jijini New York nchini Marekani jana Jumatatu.

“Wakati wa amani umewadia kwa kuwa tumesalia tu na muda mchache wa kutoweza kamwe kufikia amani,” alisema Macron muda mfupi baada ya nchi za Uingereza, Australia na Canada kutangaza kuwa pia zimelitambua taifa la Palestina.

“Ni sharti tufanye kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhifadhi uwezekano kabisa wa suluhu ya nchi mbili.  Israel na Palestina zinazoishi kwa amani na usalama.”

Nchi zingine ambazo zimetangaza kulitambua taifa la Palestina ni Luxembourg, Malta na Andorra.

Hadi kufikia sasa, mataifa zaidi ya 150 wanachama wa Umoja wa Mataifa yamelitambua taifa la Palestina.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio linaloidhinisha suluhu ya nchi mbili mapema mwezi huu.

Share This Article